Jua Cali

Jua Cali

Maelezo ya awali
Amezaliwa Septemba 12 1979 (1979-09-12) (umri 45)
Asili yake Nairobi , Kenya
Aina ya muziki Mwanamuziki
Kazi yake C E O , Mwanamuziki
Aina ya sauti "Tenor"
Miaka ya kazi 1998–mpaka sasa
Studio Calif Records
Tovuti http://www.juacali.co.ke


Jua Cali (jina lake kamili ni Paul Julius Nunda; alizaliwa Nairobi, Kenya, 12 Septemba 1979) ni mwanamuziki wa Kenya. Jua Cali ni msanii wa nyimbo za Kiswahili akitumia mtindo wa kufululiza maneno ujulikanao kama genge.

Katika mwaka 2000 yeye pamoja na Clement Rapudo (Clemo) walianzisha Calif Records ambapo Jua Cali amefanya kazi hadi sasa.

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Jua Cali alizaliwa katika eneo la Eastlands jijini Nairobi. Wazazi wake, Doreen Onditi na Evans Onditi (aliaga dunia) walikuwa waalimu. Jua Cali alilelewa katika maadili makali ya Kikatoliki mtaani California Mashariki ya jiji la Nairobi Alianza mtindo wa kufululiza maneno akiwa na umri wa miaka kumi, akitiwa moyo na kaka yake Christopher Sati. Alijulikana kama kijana aliye mnyamavu na aliyekuwa na ugumu wa kushirikiana na wenzake.

Alikuwa mwanafunzi katika shule ya msingi ya Ainsworth darasa la 1 hadi la 6 shule ya vijana ya Shepherds, Buruburu darasa la 6 hadi la 8; shule ya upili ya Jamuhuri na kisha Taasisi ya mafunzo ya viwandani ya Kenya Christian ###K#C#I#T#I Eastleigh## alikotunukiwa shahada ya ##diploma## ya teknologia ya mazulio# Katika hiyo taasisi, alishiriki katika mchezo wa ##mpira wa vikapu##, akiwa na matumaini ya kujiunga na timu ya kitaifa ya mpira wa vikapu ya ##Kenya### Hakuwahi kuweza kujiunga na hiyo timu, akisingizia urefu# Alianza mambo ya muziki kwa kujiunga na bendi ya ‘Sita Futi’ akiwa kama mwimbaji# Sita Futi ilisambaratika tu mara ilipoanzishwa, wengi wakizielekeza talanta zao za muziki kwingineko# Calif Records ilianza wakati Jua Cali na rafikiye wa utotoni ##Clemo## walipoungana na kubuni alama ya kipekee ya kurekodi , huku ikitia fora na kujulikana katika nyanja zote za muziki wa ##Afrika Mashariki### Wasanii wa Calif Records walikuwa mstari wa mbele katika orodha ya muziki na usanii# Calif Records pia ilibuni mtindo wa muziki wa ##Genge### Jua Cali humtaja kakake Chris na mamaye mzazi kama watu waliomtia moyo maishani#

Kazi ya muziki

[hariri | hariri chanzo]

Wimbo wake wa kwanza kabisa kurekodiwa ulikuwa Ruka, uliotolewa mwaka 2001 na ukafuatiwa na Nipe Asali mwaka wa 2002# Katika mwaka wa 2004 yeye na ##PiliPili## walitoa wimbo ‘Kamata Dame’# Kama wasanii wengine wa Kenya, ilimchukua miaka kadhaa kabla ya kuitoa ##albamu## yake ya kwanza kamilifu# Albamu yake ‘Juacali Sekta’ iliwahi fika sokoni mwaka wa 2006, ikizijumlisha nyimbo zake za hapo awali#

Wimbo ‘Kwaheri’ #akijumlisha ##Sanaipei### ulitia fora sana nchini Kenya mwaka wa 2007# Kwenye mkesho wa mwaka mpya 2008/2009 alitoa albamu mpya, ‘Ngeli ya Genge’# Jua Cali amezuru ##amerika## na pia mataifa mengine# Mnamo agosti 2007, alikuwa kati ya watu 100 mashuhuri nchini Kenya, hii ni kulingana na gazeti la ##The Standard###

Jina lake la uimbaji Jua Cali lilitwaliwa kutoka jina ##California##, eneo lililoko Kenya #kama katika jina Calif Records## Pia lamaanisha jua kali, jina ambalo hutumika kumaanisha viwanda vya chini katika ##uchumi## wa Kenya#

Motorola

[hariri | hariri chanzo]

Kando na kuwa na talanta ya uimbaji, amefanikiwa katika mambo ya biashara, haya yote yamechangiwa na kupendwa kwake na vijana pamoja na wale walio na umri ambao si mdogo sana. Kwa mfano, alikuwa msanii wa kwanza Mkenya kupata patano la biashara, wakati alipotia sahihi, mwaka wa 2007, patano la biashara la shilingi milioni moja za Kenya kila mwaka na kampuni kuu ya simu za rununu ya Motorola kwa ajili ya simu zake za muundo wa W. kulingana na kampuni hiyo, alikuwa mnaso mzuri kwa wateja. “ Jua Cali ni mmoja wetu katika familia ya Motorola, na tunaheshimika kwa kuwahi kufanya kazi naye hapo awali,” asema Joanne Doyle, Meneja Muuzaji katika Afrika Mashariki. “Amekuwa balozi shupavu, na kama Motorola, yeye ni mbunifu, na ana mtindo wake wa kipee, kwa hiyo tutafurahia zaidi kazi yake ngumu ikitambulika kwenye utunzi wa kifahari wa zawadi za Kisima.”

Pia amekuwa balozi wa kampuni za EABL na Safaricom

  • JUACALI SEKTA (2006)
  • NGELI YA GENGE (2008)
  • TUGANGE YAJAYO (2013)
  • MALI YA UMMA (2019)
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jua Cali kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.