Kareyce Fotso | |
Amezaliwa | Bandjoun |
---|---|
Nchi | Cameroon |
Kazi yake | Mwimbaji |
Kareyce Fotso ni mwimbaji wa Cameroon anayetumbuiza duniani kote na katika mitindo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Afro pop, blues na mangambeu. Ni mwimbaji wa kiafrika anayetunga nyimbo zake kulingana na tamaduni zilizomkuza.[1]
Fotso alizaliwa Bandjoun akakua katika mji wa Yaoundé. [2] Huko Yaoundé alijifunza kuzungumza Ewondo na mara nyingi hutumbuiza katika lugha hiyo. [2]
Fotso alisoma biokemia na filamu shuleni, lakini hatimaye aliendelea kuwa mwimbaji. [3] Fotso aliimba kwenye bendi, Korongo Jam, kuanzia mwaka 2001, hadi bendi ilipogawanyika mwaka 2006.[2] Fotso alirudi Cameroon baada ya mpasuko ambapo alianza kutumbuiza katika cabarets huko Yaoundé.[2][4] Albamu yake ya kwanza, Mulato ilitolewa ndani ya nchi mwaka 2009.[2] Mwaka 2009 Jeux de la Francophonie, alishinda medali ya fedha katika mashindano ya wimbo.[5] Mwaka 2010 aliachilia albamu yake ya, Kwegne. [4] Albamu yake iliyofata, Mokte, iliachiliwa mnamo mwaka 2014. [6]
Fotso anaimba katika mitindo mbalimbali ikijumuisha mangambeu, Afro pop, miziki ya dunia, miziki ya taratibu na miziki ya kikabila. [6] Anapoimba, mara nyingi huambatana na gitaa, ngoma za mbao au kengele [3] Fotso anatumbuiza duniani kote. [6][7]
{{cite web}}
: More than one of |accessdate=
na |access-date=
specified (help); More than one of |archivedate=
na |archive-date=
specified (help); More than one of |archiveurl=
na |archive-url=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: More than one of |accessdate=
na |access-date=
specified (help); More than one of |archivedate=
na |archive-date=
specified (help); More than one of |archiveurl=
na |archive-url=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kareyce Fotso kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |