Kolmani wa Cloyne (pia: Colmán mac Léníne; Munster, Eire 522 hivi - Cloyne, Eire, 604 hivi) alikuwa mshairi wa Kieire kwenye ikulu ya Cashel hadi alipobatizwa na Brendan akiwa tayari na umri wa miaka 48.
Baadaye alitumwa kuinjilisha eneo la Limerick na hatimaye akawa abati-askofu wa monasteri aliyoianzisha huko "Cluain Uama", leo Cloyne [1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 24 Novemba[2].
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |