“Make Me Better” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Single ya Fabolous na Ne-Yo kutoka katika albamu ya From Nothin' to Somethin' | |||||
Imetolewa | 9 Juni 2007 (ulimwenguni) | ||||
Muundo | CD single (ulimwenguni) Digital download (global) Vinyl single (North America) | ||||
Imerekodiwa | Brooklyn, New York, Marekani na Hollywood, Los Angeles, California, Marekani | ||||
Aina | Hip hop | ||||
Urefu | 4:13 | ||||
Studio | Def Jam Records | ||||
Mtunzi | John Jackson Shaffer Smith | ||||
Mtayarishaji | Timbaland | ||||
Certification | Platinum (RIAA) | ||||
Mwenendo wa single za Fabolous | |||||
|
|||||
Mwenendo wa single za Ne-Yo | |||||
|
"Make Me Better" ni single ya tatu ya msanii Fabolous' kutoka katika albamu yake ya From Nothin' to Somethin'. Wimbo umemshirikisha mwimbaji machachari wa R&B Ne-Yo, lakini alikuwa akipiga sehemu za vibwagizo tu. Wimbo umetayarishwa na Timbaland.
Timbaland alidokezea kidogo kuhusu wimbo na alisema kwamba:
Nyuzi za wimbo huu ni sampuli kutoka kwa Sherine "Al Sa'ban Aleh". Sampuli kama hii ilishawahi kutumiwa na RZA katika wimbo wa Raekwon wa mwaka 1995 ("Rainy Dayz"). Funkmaster Flex naye alishawahi kuitumia kwa ajili ya michano huru ya Busta Rhymes ya The Mix Tape Volume 1: 60 Minutes of Funk.
Wimbo huu umemfanya Fab ajikute katika hali ya kawaida, kwa kuongea na mademu. Kwa mujibu wa mashairi, Fab na Ne-Yo wanawaambia mademu zao kwamba wanalazimika kuhesabiwa kivyao — lakini wawe na mademu zao, yaani wao ni wabora zaidi.
Kwa bahati mbaya wimbo mzima ulivuja katika mtandao mnamo tar. 9 Aprili 2007.
Video yake ilitolewa mnamo tar. 23 Mei 2007. Unaweza kuitazama kwa kupitia anwani hii hapa. Roselyn Sánchez ameonekana katika video akiwa kama kipenzi cha Fabolous. Video ilianza kurushwa hewani na BET mnamo tar. 25 Mei 2007. Video hii imeuzishwa sura rapa kama Red Cafe na Dwight Freeney kama mtu aliyezinguliwa na mlevi.
Kwa kufuatana na tarehe ya kutolewa 9 Juni 2007, single ilipata kuingia katika chati za Billboard Hot 100 na kushika nafasi ya 96 na kisha baadaye 8 [1]. Single ilitumia wiki 14 kwa kushika nafasi ya kwanza katika Billboard Hot 100 Rap Tracks. Hii ni rekodi ya chati za 2006 na 2007.
Mnamo mwezi wa Januari 2008 toleo la la Gazeti la VIBE, limeipa jina kibao cha "Make Me Better" katika orodha ya nyimbo 44 bora za mwaka wa 2007[2].
Chati (2007) | Nafasi iliyoshika |
---|---|
U.S. Billboard Hot 100[1] | 8 |
U.S. Billboard Hot R&B/Hip-Hop Songs | 2 |
U.S. Billboard Hot Rap Tracks | 1 |
U.S. Billboard Pop 100 | 14 |
Canadian Hot 100 | 79 |