Mashahidi wa Douai ni jina linalotumiwa na Kanisa Katoliki kujumlisha mapadri 160 hivi waliojiandaa huko Douai (Ufaransa) kwenda au kurudi Uingereza au Wales ili kufanya utume huko, bila kujali dhuluma kali ya serikali ya nchi hiyo dhidi ya Wakatoliki.
Kwa ajili hiyo waliuawa kati ya miaka 1577 na 1680 kama wasaliti.[1]
Kati yao, zaidi ya 80 walitangazwa wenye heri na Papa Pius XI tarehe 15 Desemba 1929 pamoja na wafiadini wengine wa dhuluma hiyohiyo. Baadhi yao walitangazwa na Papa Paulo VI kuwa watakatifu tarehe 25 Oktoba 1970.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 4 Mei au 25 Oktoba[2].
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mashahidi wa Douai kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |