Miguel Pedro Ho Ferrão (alizaliwa 16 Januari 1996) Ni mchezaji wa mpira wa Kikapu kutoka Afrika Kusini-Ureno wa Cape Town Tigers. Mzaliwa wa Johannesburg, Afrika Kusini, anaiwakilisha Ureno kimataifa.
Ferrão alicheza miaka ya kwanza ya uchezaji wake na Egoli Magic ya Ligi ya Kitaifa ya Mpira wa Kikapu (BNL). Katika fainali ya msimu wa 2020–21, alikuwa na pointi 25 na baundi 21 na alitajwa kuwa MVP wa ligi[1].
Tangu 2021, yuko kwenye orodha ya Cape Town Tigers.[2]
Ferrão amecheza na timu ya Ureno ya walio chini ya umri wa miaka 18 na chini ya miaka 20 katika Mashindano yao ya Uropa katika kitengo B.[3]