Norbert Zongo | |
---|---|
| |
Jina la kuzaliwa | Norbert Zongo |
Alizaliwa | Julai, 1949 Koudougou |
Alikufa | 13 Desemba 1998 |
Nchi | Burkina Faso |
Kazi yake | Mwandishi wa habari. |
Norbert Zongo (mwezi wa Julai 1949, Koudougou - 13 Desemba 1998) alikuwa mhariri na mchapishaji wa gazeti la l'Indépendant la nchini Burkina Faso. Zongo aliuawa baada ya gazeti lake kuanza kufanya uchunguzi juu ya mauaji ya dereva aliyekuwa anafanya kazi kwa ndugu wa rais Blaise Compaoré.
Mnamo tarehe 13 Desemba ya mwaka 1998, mwili wa Zongo ulikutwa umeungzwa pamoja na ndugu zake wengine, akiwemo Ernest Zongo, Ablasse Nikiema, na Blaise Ilboudo. Maiti hizo zilikutwa ndani ya gari karibu kidogo na mji wa Sapouy, km 100 kusini mwa mji mkuu wa Ouagadougou.
Tume huru ya uchunguzi ilitamka kwamba Norbert Zongo aliuawa kwasababu za kisiasa, kwakuwa alikuwa akifanya kazi ya upepelezi juu ya aliyekuwa dereva wa ndugu wa rais Blaise Compaoré, David Ouedraogo.
Mnamo Januari ya mwaka wa 1999, Francois Compaoré, ndugu wa rais Blaise Compaoré', alishtakiwa kwa kosa la mauaji na kuutupa baharini mwili wa mhanga bwana David Ouedraogo, dereva wake, ambaye majibu ya kifo chake yanaonyesha kwamba alikufa kwa kuteswa mnamo Januari mwaka 1998. Mashtaka baadae yaliamuliwa na sheria za kijeshi baada ya Francois Compaoré kukata rufaa dhidi yao.
Mnamo Agosti mwaka 2000, wanausalama watano wa rais, walishtakiwa kwa kosa la mauji ya Ouedraogo. Watu hao ni Marcel Kafando, Edmond Koama na Ousseini Yaro, ambaye pia anatuhumiwa katika kesi ya Norbert Zongo, huyo alifungwa kifungo cha maisha. Mwingine ni Edmond Koama ambaye alikufa mnamo tarehe 4 Januari ya mwaka wa 2001.
Mwimbaji Alpha Blondy alitunga nyimbo iliyoitwa "Journalistes en danger" kuhusu mauaji ya Norbert Zongo.
Mnamo 19 Julai, mashtaka yaliamuliwa upande katika upande wa kesi ya Zongo ambapo aliyehukumiwa alikuwa bwana Marcel Kafando.
Zongo pia aliwakuwa mtunzi wa vitabu, moja kati ya vitabu vyake baadae vilitafsiriwa kwa Kiingereza na kiliitwa The Parachute Drop, kitabu ambacho kilichapishwa na Africa World Press mnamo 2004.
Mifano yake ya kiandishi pia ilitafsiriwa kwa Kiingereza na inaweza kupatikana katika baadhi ya makala iliyoitwa "The Mobutuization of Burkina Faso". Zongo alikuwa akifanya shuguli nyingi tu za kiandishi, ikiwemo utafsiri, lugha, uhariri na uchapishaji.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Norbert Zongo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |