Perfekto (alifariki Cordoba, Hispania, 18 Aprili 850) alikuwa padri wa Cordoba aliyefungwa na hatimaye kuuawa kwa upanga na Waislamu waliotawala nchi hiyo kwa sababu aliungama kwa imara hadharani imani yake ya Kikristo na kupinga mafundisho ya Kiislamu [1] [2].
Taarifa zake ziliandikwa na Eulogi wa Kordoba[3] [4].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 18 Aprili[5].
![]() |
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |