Placidus Gervasius Nkalanga, O.S.B. (19 Juni 1919 - 18 Desemba 2015) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania.
Aliwekwa wakfu na Papa Yohane XXIII mwaka 1961.
Tangu 1969 alikuwa askofu wa Jimbo la Bukoba hadi 1973 alipojiuzulu ili kujiunga na utawa wa Wabenedikto huko Hanga (Songea) alipoishi hadi kifo chake.
Aliwahi kuwa rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (1969-1970).
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |