Kampuni ya Viatu ya Red Wing | |
---|---|
Jina la kampuni | Kampuni ya Viatu ya Red Wing |
Ilianzishwa | 1905 |
Mwanzilishi | Charles H. Beckman |
Huduma zinazowasilishwa | Utengenezaji |
Aina ya kampuni | Kampuni ya Kibinafsi Kampuni ya kimataifa |
Makao Makuu ya kampuni | Red Wing, Minnesota |
Bidhaa zinazosambazwa na kampuni hii | Viatu |
Tovuti | http://www.redwingshoes.com |
Red Wing Shoes ni kampuni ya viatu iliyokuwa na makao yake mjini Red Wing, Minnesota katika nchi ya Marekani. Ilianzishwa katika mwaka wa 1905 na Charles H Beckman.
Baada ya miaka kumi tu ya kuanzishwa kwake,kampuni ya Red Wing ilikuwa inazalisha zaidi ya jozi 200,000 za viatu kila mwaka na ikawa kampuni ya kimsingi ya kutengeneza viatu vya wanajeshi wa Marekani katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Kampuni ya Red Wing iliendelea katika mienendo yake ya kutengeneza viatu vya vita ilipotengenezea jeshi la Marekani viatu vya Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
Ingawa Red Wing inajulikana sana kwa viatu vyao vya ngozi vya kutumika katika kazi ngumu, kampuni hii imepanua viatu vinavyotengenezwa na kuwa na viatu vya mitindo ya spoti na vile vya kazi maalum. Viatu hivi ni kama viatu visivyoteleza (kutumika katika sekta ya huduma) na viatu vya kulinda vidole vya miguu(vinavyotumika katika sekta ya kuchimbua madini). Kampuni inazalisha pia viatu vya aina ya oxford, ya chukka, viatu vya kupanda milima na vya mitindo ya wakata miti (hasa viatu vya inchi 6 na inchi 8).
Ili kufuata viwango vya utengeneaji vya ASTM F 2413-05 na vya MI/75 C/75, Kampuni ya Red Wing huunda viatu vyao vingi vikiwa na chuma na vingine alumini na pia soli zisizodungika ili kuhitimu kiwango cha ASTM F 2413-05. Red Wing, pia, huunda viatu vyenye uwezo wa kupoteza nguvu za umeme hasa ili kupunguza kiasi cha umeme kinachopita kwa mwili wa mtu iwapo mtu huyo atagusa nyaya kavu za stima.Hii pia inasaidia kwa kumpa mtu ulinzi kutoka kukanyaga au kugusa kiajali vitu vilivyokuwa na stima.
Licha ya kutengeneza viatu chini ya jina lao la Red Wing,kampuni hii inaunda viatu chini ya majina mengine kama Carhartt, Irish Setter, Vasque na Worx. Katika mwaka wa 2008, Kampuni ya Red Wing ilianza kuunda viatu chini ya jina la Red Wing Heritage Lifestyle.Miundo yake mipya ikiwa ikitumia mitindo ile ya kitambo ya viatu vya karne zilizopita.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Red Wing Shoes kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |