Rudolf Sherwin

Rudolf Sherwin (Rodsley, Derbyshire, 25 Oktoba, 1550Tyburn, 1 Desemba 1581) alikuwa padri wa Uingereza maarufu kwa akili na imani[1].

Mwaka mmoja baada ya kupata digrii ya pili aliacha ushirika wa Anglikana ili kujiunga na Kanisa Katoliki, alipata upadrisho huko Ufaransa mwaka 1577, alikwenda Roma alikokaa miaka 3[2], halafu akatumwa kwao alipofanya utume kwa siri miezi michache tu[3].

Alipokuwa gerezani mwaka mzima aliongoa wengi na hatimaye alinyongwa na kukatwa vipandevipande. Maneno yake ya mwisho yalikuwa: "Iesu, Iesu, Iesu, esto mihi Iesus!"[4].

Alitangazwa mwenye heri na Papa Pius IX mwaka 1929 na mtakatifu mwaka 1976 na Papa Paulo VI.

Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki tarehe 1 Desemba[5].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/93208
  2. ""Douai, Ordination, and Rome", Saint Ralph Sherwin". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-12-09. Iliwekwa mnamo 2020-11-29.
  3. "St. Ralph Sherwin" by Father Robert F. McNamara Ilihifadhiwa 1 Machi 2018 kwenye Wayback Machine. Retrieved on 1 Mar 2018
  4. "Blessed Ralph Sherwin". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913. http://www.newadvent.org/cathen/12636b.htm.. Accessed 2011-10-18.
  5. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.