Shelton Johnson (alizaliwa Detroit, Michigan, 1958) ni mlinzi wa mbuga chini ya Huduma ya Hifadhi za Taifa ya Marekani, na anafanya kazi katika Hifadhi ya Kitaifa ya Yosemite. Kufikia mwaka 2021 alikuwa amefanya kazi Yosemite kwa miaka 28 kati ya miaka yake 35 ya kufanya kazi.
Johnson alianza kazi yake katika Hifadhi ya Kitaifa ya Yellowstone mwaka 1987.[1] Alionekana mara nyingi katika kipindi cha Ken Burns The National Parks: America's Best Idea, kilichotangazwa kwenye PBS Septemba 27 hadi Oktoba 2, 2009, na aliitwa "nyota asiyetarajiwa" wa filamu hiyo.[2]
Johnson alihudhuria onyesho la kukagua filamu hiyo katika Ikulu ya Marekani siku hiyo, ambapo alijadili filamu hiyo na Rais Barack Obama.[3]
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Shelton Johnson kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |