Silver Ayoo

Silver Ayoo (alizaliwa 26 Novemba 1950) ni mwanariadha wa zamani wa Uganda ambaye alishindana kama mwanariadha katika mbio za mita 400. Aliiwakilisha Uganda katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto mwaka 1972 na 1980.

Ayoo alishiriki katika mbio za mita 400 katika Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto mwaka 1972 na aliondolewa katika mbio za ufunguzi.[1]

Katika Michezo ya Africa Nzima mwaka 1973 huko Lagos, Ayoo alishinda medali ya shaba katika mbio za mita 400 kuruka viunzi.[2]

Ayoo alishinda medali ya fedha na shaba katika Michezo ya Jumuiya ya Madola ya Uingereza mwaka 1974, katika mbio za mita 400 na 4 x 400 mtawalia.[3]

Alikosa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto mwaka 1976 kwani Uganda ilikuwa mojawapo ya nchi zilizosusia.[4]

Akiwa amerudi kwenye Michezo ya Olimpiki mwaka 1980 aliboresha kiwango chake cha awali katika mbio za mita 400 kwa kutinga robo fainali. Pia alikuwa mwanachama wa timu ya Uganda ya mbio za mita 4 × 400 katika michezo hiyo.[5]

  1. "Results of Olympics", The Morning News, 4 September 1972, p. 25. Retrieved on 4 October 2016. 
  2. Zziwa, Hassan Badru. "Kiprotich glory and how forces transformed Ugandan sport", The Observer, 26 August 2012. Retrieved on 4 October 2016. 
  3. Lumu, David. "Finally, a defining moment for Kipsiro", The Observer, 10 October 2010. Retrieved on 4 October 2016. 
  4. "Pembroke signs 4", Star-News, 8 September 1976, pp. 3–C. Retrieved on 4 October 2016. 
  5. Kyeyune, Darren Allan. "Sixteen years later, Olympic Games jinx still hovers over Uganda", Daily Monitor, 21 July 2012. Retrieved on 4 October 2016. 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Silver Ayoo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.