Sofia Kawawa

Sofia Kawawa

Sofia Kawawa

Chairman Union of Women of Tanzania

tarehe ya kuzaliwa 12 August 1936
Masonya Village, Tunduru, Ruvuma
tarehe ya kufa 11 Februari 1994 (umri 57)
Moshi, Kilimanjaro, Tanzania
mahali pa kuzikiwa Madale Dar es Salaam
utaifa Tanzanian
chama TANU, CCM
ndoa Rashid Mfaume Kawawa (m. 1951)
watoto 8
taaluma Activist/politician

Sofia Kawawa (jina la awali: Selemani Mkwela, 12 Agosti 19361994) alikuwa mwanzilishi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT). Alikuwa mwanachama wa chama cha Tanganyika African National Union (TANU) na baadaye Chama cha Mapinduzi (CCM).

Maisha ya zamani

[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa kijiji cha Masonya wilaya ya Tunduru mkoa wa Ruvuma. Alisoma shule ya msingi ya Masonya na baadaye akamaliza elimu yake ya msingi mkoani Tabora . Mnamo mwaka 1951 aliolewa na Rashid Kawawa ambaye alikua Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanganyika / Tanzania .

Alikuwa miongoni mwa mwanamke wa kwanza kujiunga na Chama cha TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika. Alianzisha Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) pamoja na Bibi Titi Mohamed na kuendelea kuwa mwenyekiti wa pili kuanzia 1980 hadi 1990. Wanawake hao wawili walikuwa wanaharakati wa kwanza kutetea haki za wanawake nchini na walipanda mbegu hata kabla yakupata uhuru.

Maoni ya kifalsafa na kisiasa

[hariri | hariri chanzo]

Mama Kawawa na wanaharakati wengine walikuwa na kauli mbiu isemayo "Lazima iwe kutoka mashina ya chini". Alifanya kampeni kwa wanawake kuwa viongozi. Aliwasaidia Anna Abdallah na Gertrude Mongella kuwa wabunge.

Haya ni matunda ya kazi yake ya kupanda mbegu ya usawa 50/50 ambayo leo wanaharakati na wanasiasa wanataka ushiriki wa wanawake na wanaume uwe 50/50.

Kazi zilizochapishwa

[hariri | hariri chanzo]
  • Wanamgambo, Akina Mama, na Familia ya Kitaifa(Militants, Mothers, and the National Family)