Supamaketi za Uchumi

Supamaketi za Uchumi
Ilipoanzishwa1975
Makao MakuuNairobi
Tovuti[1]
Nembo ya Supamaketi za Uchumi

Supamaketi za Uchumi (kifupi: Uchumi) ni mtandao wa supamaketi nchini Kenya ulioanzishwa mwaka wa 1975 na uliorodheshwa katika Soko la Hisa la Nairobi mwaka wa 1992. [1]

Kufungwa na kufunguliwa tena

[hariri | hariri chanzo]

Uchumi ilifungwa, kwa muda, katika mwezi wa Juni 2006 baada ya miaka 30 ya biashara. [2] Wakati huo kufungwa kwake kulionekana kama msiba mkubwa zaidi uliokumba biashara katika historia ya Kenya. [3] Baadaye serikali ilianzisha mpango wa kuiokoa na hapo basi vituo vitano vya Uchumi vikafunguliwa tena tarehe 15 Julai 2006, vyote vikiwa Nairobi.

Hali ya sasa

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Januari 2015 Uchumi ilikuwa ikiendesha maduka 37 nchini Kenya. Yaliyowahi kufunguliwa nje ya nchi yamefungwa yote.

Kampuni ina wenye hisa 12,000 hivi baada ya kurudishwa kwa kampuni kwenye soko la hisa la Nairobi.[4]

Wafanyakazi wake ni 50 (2022) na mtaji ni wa dola 78.8 milioni (2014).

Angalia pia

[hariri | hariri chanzo]
  • Nakumatt, mshindani wa Uchumi nchini Kenya

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Uchumi prunes unprofitable branches". 10 Februari 2005. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-09-11. Iliwekwa mnamo 2006-06-04.
  2. "Kenyan shop chain shuts its doors". BBC News. 2 Juni 2006. Iliwekwa mnamo 2006-06-04.
  3. "Editorial: Pending queries on fall of Uchumi". The Standard online. 3 Juni 2006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-10-07. Iliwekwa mnamo 2006-06-04.
  4. http://allafrica.com/stories/201011090254.html
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Supamaketi za Uchumi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.