Terror Squad (studio) | |
---|---|
Shina la studio | EMI |
Imeanzishwa | 1992 |
Mwanzilishi | Fat Joe |
Usambazaji wa studio | Virgin Records |
Aina za muziki | Hip hop |
Nchi | Marekani |
Mahala | The Bronx, New York |
Terror Squad (zamani iliitwa Terror Squad Entertainment) ni studio ya kurekodia muziki wa hip hop na R&B iliyoanzishwa na msanii wa hip hop maarufu kama Fat Joe, mjini The Bronx, New York, Marekani.
Studio ilianzishwa mnamo mwaka wa 1992. Kazi za studio hiyo zilikuwa zikisambazwa na studio ya Relativity Records na Atlantic Records, lakini sasa, kazi za DJ Khaled zinasambazwa na studio ya Imperial Records na Virgin Records ya EMI.