United People's Democratic Party (UPDP) ni chama cha siasa nchini Tanzania kilichosajiliwa rasmi tarehe 4 Februari 1993.
Katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 chama hakikumsimamisha mgombea wa kiti cha urais na badala yake kilimuunga mkono mgombea wa chama cha National Convention for Construction and Reform-Mageuzi (NCCR-Mageuzi) kilichomsimamisha Sengondo Mvungi ambaye alipata asilimia 0.49% ya kura zote
Katika uchaguzi wa mwaka 2015 kilimsimamisha Fahmi Dovutwa kama mgombea wa urais.[1]