Uwanja wa michezo wa Afraha

Uwanja wa michezo wa Afraha ni uwanja wa michezo wenye matumizi mengi na unapatikana Nakuru, nchini Kenya. Unatumika zaidi na chama cha mpira wa miguu na pia ni uwanja wa nyumbani wa timu ya Nakuru AllStars inayoshiriki ligi kuu Kenya; pia Ulinzi Stars wanaoshiriki ligi kuu nchini humo wanautumia pia. Uwanja unachukua takribani watu 8,200 (Elfu nane na mia mbili) na ulifunguliwa mnamo mwaka 1948.

Uwanja huo uko umbali wa kilomita mbili kutoka Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Nakuru. Ingawa ni uwanja wa mpira, ulifahamika kwa kuandaa mikutano mingi ya kisiasa ikiwa ni pamoja na GEMA waliokua wakiimiza mabadiliko ya safu ya katiba iliyofanyika mwaka 1970. Chama tawala cha zamani KANU pia kilifanya mikutano mingi mashuhuri.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Afraha kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.