Wolfgang Lukschy | |
---|---|
Amezaliwa | 19 Oktoba 1905 Berlin, Ujerumani |
Amekufa | 10 Julai 1983 |
Miaka ya kazi | 1940 - 1979 |
Wolfgang Lukschy (19 Oktoba 1905 - 10 Julai 1983 mjini Berlin) alikuwa mwigizaji wa filamu na na muundaji wa rekodi za muziki wa filamu kutoka nchini Ujerumani. Huyu, alishawahi kutumbuiza katika maukumbi, filamu, na vipindi vya televisheni (tamthilia).
Amecheza zaidi ya filamu 75 pamoja na kuonekana katika vipindi vya TV kunako miaka ya 1940 na 1979. Inawezekana akawa ameanza kufahamika zaidi baada ya kucheza kama Alfred Jodi katika filamu ya kivita ya Kimarekani mnamo mwaka wa 1962 ya The Longest Day. Pia anajulikana zaidi kwa kucheza kama John Baxter katika mkusanyika wa kwanza wa filamu iliyoongozwa na Sergio Leone ya A Fistful of Dollars kunako 1964, akiwa sambamba kabisa na Clint Eastwood na Gian Maria Volontè.
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wolfgang Lukschy kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |