Yu Xiaogang (Kichina: 于晓刚; pinyin: Yú Xiǎogāng) ni mwanamazingira nchini China. Alitunukiwa Tuzo ya Mazingira ya Goldman mnamo mwaka 2006 kwa juhudi zake za kuunda programu za usimamizi wa vyanzo vya maji wakati akitafiti na kuweka kumbukumbu juu ya athari za kijamii na kiuchumi ambazo mabwawa yalikuwa nayo kwa jamii za ndani za Wachina.[1]Yeye ni miongoni mwa washindi sita wa Tuzo za Ramon Magsaysay mnamo mwaka 2009, zinazochukuliwa na wengi kuwa sawa na Waasia wa tuzo ya Nobel. Alimaliza Shahada yake ya Uzamili kutoka Taasisi ya Teknolojia ya Asia(AIT) nchini Thailand.