Zithulele Patrick Mvemve

Zithulele Patrick Mvemve (31 Mei 19416 Julai 2020) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki la Afrika Kusini.

Mvemve alizaliwa Evaton, Afrika Kusini, na alilelewa katika Shule ya Upili ya St. Martin de Porres huko Soweto. Alisomea upadre katika Seminari ya St. Peter's huko Hammanskraal, Pretoria.

Alitunukiwa daraja ya upadri mnamo 1969. Alikuwa askofu msaidizi wa Askofu Mkuu wa Johannesburg na askofu wa Luperciani kutoka 1988 hadi 1994, na baadaye aliteuliwa kuwa askofu wa Jimbo la Klerksdorp, Afrika Kusini, kutoka 1994 hadi 2013.[1]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.