Awilo Longomba | |
---|---|
Jina la kuzaliwa | Albert William Louis Longomba |
Amezaliwa | 5 Mei 1962 |
Kazi yake | Mwimbaji, drama |
Ameshirikiana na | Viva la Musica, Loketo, Dindo Yogo, Luciana Demingongo |
Awilo Longomba (5 Mei, 1962) ni mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambaye alikuwa mpiga dramzi katika bendi mbalimbali tangu miaka ya 1980. Bendi alizofanya nazo kazi ni pamoja na Viva la Musica, Stukas, Nouvelle Generation na Loketo.
Mwaka wa 1995, hatimaye aliacha kupiga dramzi na kuamua kuimba. Akatoa albamu yake ya kwanza, Moto Pamba. Ni baada ya kupata msaada kutoka kwa Shimita, Ballou Canta, Dindo Yogo, Dally Kimoko, Sam Mangwana, Syran Mbenza na Rigo Star.
CD yake ya pili, Coupe Bibamba (mwaka wa 1998) ilimfanya ajulikane kote barani Afrika, pia Ulaya na Amerika. Hii ilifuatiwa na Kafou Kafou (mwaka wa 2001) na Mondongo (mwaka wa 2004), ambayo inawashirikisha Japponais, Dally Kimoko, Caen Madoka, Djudjuchet, Josky na Simaro Lutumba. Pia alishirikishwa kama atalaku (mtu wa kutumbuiza) katika baadhi ya rekodi za soukous.
Mnamo 2008 Awilo Longomba alitoa albamu mpya, Super-Man, ambayo ilikuwa fanikio lingine kubwa. Awilo aliendelea na umaarufu wake nchini Marekani / Kanada huku akiwa katika ziara pamoja na Nabtry International Cultural Dancers (kundi la kitamaduni la kimataifa la kusakata au kucheza ngoma) kundi la Kiafrika ya kucheza ngoma iliyoanzishwa mwaka wa 2007 na Grace Haukwa. Ziara ya Super-Man ilikuwa yenye mafanikio makuu miaka za 2008 na 2009. Kutokana na kura za umaarufu na ushindi wa kihistoria katika Tuzo za Reggae ya Kimataifa na Muziki wa ulimwengu huku nchi zaidi ya 120 zikipiga kura, albamu mpya ya Awilo, Super-Man, ilishinda tuzo ya mtumbuizaji bora wa Soukous wa mwaka 2009.
Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa Nabtry Grace Haukwa ambaye anamwakilisha Awilo nchini USA alikuwepo kupokea tuzo hilo kwa niaba ya Awilo katika sherehe ya Tuzo za Reggae ya Kimataifa na Muziki wa ulimwengu.
Awilo kwa sasa anaishi nchini Uingereza katika jiji la London, Uingereza. Amemwoa Paradis Kacharelle ana wana mtoto wa kiume aitwaye Lovy Believe Church Awilo Longomba.
Ndugu wa Awilo katika tasnia ya muziki ni pamoja na baba yake Victor Longomba aliyekuwa mwanachama mwanzilishi wa TP OK Jazz na vilevile Longombas ambalo ni kundi maarufu la Afro-fusion lenye makao nchini Kenya.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Awilo Longomba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |