Leodgar Tenga ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu kutokea nchini Tanzania. Aliichezea Tanzania katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya maka 1980. Baada ya kustaafu, alishika wadhifa wa raisi wa Shirikisho la Soka Tanzania kuanzia mwaka 2004 hadi 2013. Wakati wa uongozi wake, Tenga alichaguliwa kuhudumu kama rais wa CECAFA mwaka 2007 na alichaguliwa tena mwaka 2011 kwa muhula wa pili. Alikuwa mwanachama wa Kamati ya Utendaji ya CAF chini ya Rais wa zamani Ahmad Ahmad kati ya 2017 na 2021.[1][2]
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Leodgar Tenga kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |