Levy Sekgapane (alizaliwa 16 Desemba, 1990), ni mwimbaji wa nchini Afrika Kusini ambaye pia hufanya majukumu mengine katika G. Rossini, G. Donizetti, WA Mozart na JS Bach .
Levy Sekgapane alizaliwa mnamo tarehe 16 Desemba mwaka 1990 huko Kroonstad, Afrika Kusini. Alihitimu masuala ya muziki katika Chuo Kikuu cha Cape Town . [1][2]
Levy Sekgapane alipata tuzo ya 1 katika shindano la International Hans Gabor Belvedere Singing Competition [3] na pia tuzo ya 1 katika shindano la Kimataifa la kuimba la Montserrat Cabalé mnamo mwaka 2015. Katika majira ya joto ya mwaka 2017, alishinda tuzo ya 1 katika Operalia ya Plácido Domingo, Mashindano ya Opera ya Dunia. [4]
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Levy Sekgapane kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |