Victor Longomba Besange Lokuli, anayejulikana kwa jina la Vicky Longomba. (13 Desemba 1932 – 12 Machi 1988 huko Kinshasa[1] ) alikuwa mwimbaji na mwanachama mwanzilishi wa Tout puissant OK Jazz, kikundi cha rumba cha Kongo.[2][3]
Baadaye alianzisha kundi lake la Lovy du Zaire.
Alikuwa babake Lovy Longomba (mwanachama wa Super Mazembe) na Awilo Longomba, wote wanamuziki maarufu.