Visenti Liem Pham Hieu, O.P. (1731-1773) alikuwa padri wa Vietnam aliyekamilisha juhudi zake kwa uenezaji wa Injili kwa kukatwa kichwa pamoja na padri Mdominiko mwenzake Yasinto Castenyeda wakati wa dhuluma ya kaisari Trịn Sam[1]
Ni kati ya Wakristo wafiadini wa Vietnam waliouawa kwa ajili ya imani yao huko Vietnam katika karne ya 17, 18 na 19 (1625–1886).
Wanatajwa pia kama Watakatifu Andrea Dũng-Lạc na wenzake 116.
Kwa nyakati tofauti, Papa Leo XIII, Papa Pius X na Papa Pius XII waliwatangaza kuwa wenye heri, halafu Papa Yohane Paulo II aliwaunganisha katika kuwafanya watakatifu wafiadini tarehe 19 Juni 1988.
Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 24 Novemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 7 Novemba [2].
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |