Harmonize | |
---|---|
Msanii wa muziki wa Bongo Flava nchini Tanzania | |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Rajab Abdul Kahali |
Pia anajulikana kama | Harmonize |
Asili yake | Mtwara,Tanzania |
Aina ya muziki | Bongo Flava,Afro Pop |
Kazi yake | Mwimbaji-mtunzi, mtayarishaji wa rekodi |
Ala | Piano, sauti |
Miaka ya kazi | 2011–mpaka sasa |
Studio | KONDE MUSIC WORLDWIDE |
Ame/Wameshirikiana na | Rayvanny, Diamond Platnumz |
Tovuti | Tovuti Halisi |
Harmonize (kwa jina lake halisi Rajab Abdul Kahali; mara kadhaa hujiita "Konde Boy"; amezaliwa Chitoholi, mkoa wa Mtwara ni mwimbaji na mtunzi wa muziki kutoka Tanzania.
Alianza kuvuma kwa kibao chake cha kwanza "Aiyola" (2015), Bado (2016), Matatizo (2016) na baadaye akatoa nyimbo na msanii mwenzie kutoka lebo moja ya WCB (Wasafi Classic Baby) ambaye ni Diamond Platnumz.
Aliamua kuhama WCB na kuanzisha lebo yake Konde Music Worldwide [1].
Kwa ngwaru ni wimbo ambao ulibamba karibia maeneo yote ya Afrika ya Mashariki akatoa kibao kingine kiitwacho inama nyimbo ambayo aliimba na msanii kutoka nje ya Tanzania ambaye anaitwa burna na diamond Platnumz alikuwepo kwenye huo wimbo. Sasa hivi anatamba na kibao kiitwacho Never Give Up, wimbo ambao unaelezea historia ya maisha yake kuanzia alivyo kuwa na maisha magumu sana. Harmonize anasimamiwa na Joel Joseph au kwa jina lingine Mr Puaz. Kwa sasa msanii huyu yuko peke yake baada ya kujitoa WCB pia amekuwa akitoa ngoma kama vile uno ambayo imepata umaarufu mkubwa na kuwa gumzo yani number one on trending. Pia kwa sasa ameachia kazi yake ya pili iitayo kushoto kulia ambayo amesikika akimtaja Diamond ambapo ni kwa mara ya pili.
Harmonize ana asili ya Mtwara. Alisoma katika shule ya sekondari Mkundi iliyopo mjini Mtwara. Baada ya kumaliza elimu yake ya sekondari, Harmonize alielekea Dar es Salaam ambako alijipatia riziki yake ya kila siku.
Harmonize mwanzoni alibeba maji ili kupata tonge la chakula, pia alikuwa akiuza kahawa kwa wafanyabiashara wengine na wakazi wa Kariakoo jijini Dar es Salaam kabla ya sauti yake kutambulika mitaani. Kisha kuchukuliwa na lebo ya Diamond Platnumz ijulikanayo kama WCB. Kwa sasa ameamua kujiondoa katika lebo hiyo kutokana na sababu ambazo hazikuwekwa wazi.
Alianza kujihusisha na muziki mnamo mwaka 2011 ambapo alitoa nyimbo mbalimbali lakini hazikuweza kupata umaarufu mkubwa mpaka pale ambapo alikutana na Diamond Platinumz mnamo mwaka 2015 na kuanza kufanya muziki pamoja naye.
Harmonize ndiye mwanamuziki aliyetoa albamu yenye nyimbo 18 akiwa amewashirikisha Yemi Alade wa Nigeria na albamu hiyo inaitwa Afro East.
Nambari | Mada ya wimbo | Mwaka |
---|---|---|
1. | Aiyola | 2015[1] |
2. | Bado ft Diamond Platnumz | 2016 |
3. | Matatizo | 2017 |
4. | Happy Birthday | 2017 |
5. | Shula | 2017 |
6. | Sina | 2017 |
7. | Niambie | 2017 |
8. | Dont go | 2017 |
9. | Nishachoka | 2017 |
10. | Nakupenda | 2017 |
11. | Kwa ngwaru ft. Diamond platnumz | 2018 |
12. | Dm chick | 2018 |
13. | Atarudi | 2018 |
14. | Paranawe ft. Rayvanny | 2018 |
15. | Niteke | 2019 |
16. | Show me what you gat ft. Yemi Alade | 2019 |
17. | Kainama ft. Diamond Platnumz na Burna boy | 2019 |
18. | Ndoenda | 2019 |
19. | Never give up | 2019 |
|20. |Mdomo |2021
Mwaka | Kazi iliyoteuliwa | Tuzo | Matokeo |
---|---|---|---|
2016 | Bado Ft Diamond Platnumz | WatsUp TV Tuzo la Video Bora zaidi ya Mwimbaji Chipukizi | Ameshinda[2] |
Yeye Mwenyewe | African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) kwa Mwimbaji Chipukizi | Ameshinda[3] | |
African Entertainment Awards (AEAUSA) kwa Msanii Chipukizi Bora zaidi | Ameshinda[4] |
2022 kilimanjaro Tanzania music arward= best male artist
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Harmonize kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |